Tuesday, 14 October 2014

Kuumia kwa Ozil si tatizo kwa Arsenal-Wilshere.

Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere haamini kuwa kuumia kwa  Mesut Ozil ni athari kubwa kwa klabu yao ya Arsenal inayojiandaa kucheza na  Hull City  katika ligi kuu ya Uingereza.

Mjerumani huyo atakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya kuumia goti na amekuwa mchezaji muhimu katika msimu huu wa 2014-15.

Taarifa zilizonaswa na mtandao huu ni kwamba  Wilshere amesema kuwa nafasi ya Ozil itazibwa na  Alex Oxlade-Chamberlain na Theo Walcott, ambaye kwa sasa amepona.

"Ozil anacheza upande wa kushoto,atakaa mtu yeyote,"alisema Wilshere.

"Chambo atatumia hiyo nafasi. Theo amepona. Kwa hiyo  Theo au Chambo atacheza tu alisema Wilshere.

Ameendelea kusema kuwa kuna wachezaji wengi tu ambao wana uwezo wa kucheza namba 10 kama Ozil.

Ikumbukwe kuwa Ozil atakosa baadhi ya mechi ndani ya Arsenal
ambazo  ni
18 October: Hull (H) - Premier League

22 October: Anderlecht (A) - Champions League

25 October: Sunderland (A) - Premier League

1 November: Burnley (H) - Premier League

4 November: Anderlecht (H) - Champions League

9 November: Swansea (A) - Premier League

22 November: Man Utd (H) - Premier League

26 November: Borussia Dortmund (H) - Champions League

29 November: West Brom (A) - Premier
3 December: Southampton (H) - Premier League

6 December: Stoke (A) - Premier League

9 December: Galatasaray (A) - Champions League

13 December: Newcastle (H) - Premier League

21 December: Liverpool (A) - Premier League

26 December: QPR (H) - Premier League

28 December: West Ham (A) - Premier League.

0 comments:

Post a Comment