Thursday, 2 October 2014

Mbeya City yapata udhamini wa Coca-Cola Kwanza.

Klabu  ya Mbeya City Leo hii imeingia makubaliano na Kampuni ya Coca-Cola kwanza ya udhamini wa Miaka Miwili wenye thamani ya Shilingi Milioni 150.

Kwa mujibu wa Taarifa maalum ya Mbeya City Mkataba huo wa udhamini upo katika maeneo makubwa mawili ambayo ni vinywaji, yaani Maji aina ya Dasani wakati wa mazoezi na mashindano, pamoja na vinywaji vingine kulingana na mahitaji ya Klabu vitakavyokuwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 na pia Fedha taslimu Shilingi Milioni 60 kwa Mwaka.

Taarifa hiyo ya Mbeya City imetoa shukrani kubwa kwa Kampuni ya Coca-Cola kwanza  kwa imani yao kwao na wao wameahidi kuongeza bidii ili wao na Wanamichezo wengine Nchini wanufaike kwa fursa za aina hii.
MBEYA-CITY-SIGNING-COCA2Taarifa hiyo ilimaliza kwa kuwaomba Wapenzi wao wote kuwa Mabalozi wazuri kwa kutumia kinywaji baridi cha Kampuni ya  Coca-Cola kwanza.

0 comments:

Post a Comment