Wednesday, 19 November 2014

Kufa au kupona AFCON leo,Nchi 7 zinasubiriwa kufuzu

Nigeria ambao ni mabingwa watetezi leo wataongoza timu kongwe wakiwemo mabingwa mara nne Ghana na Ivory Coast katika mechi za mwisho za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika Guinea ya Ikweta.

Nigeria ambao walifufua matumaini yao ya kufuzu mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuichapa Congo Brazzaville sasa wanakabiliwa na kibarua cha kuhakikisha watawafunga vinara katika kundi A Afrika Kusini katika mchezo utakaofanyika katika uwanja mpya wa Akwa Ibom huko Uyo ili kujihakikishia nafasi hiyo.

Afrika Kusini ambao walikuwa mabingwa wa Afcon mwaka 1996 hawajafungwa katika mechi zao tano walizocheza lakini watakwenda Uyo huku wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kushinda mara moja katika mechi 10 walizocheza na Nigeria.

Congo ambao mara ya mwisho walicheza michuano hiyo miaka 14 iliyopita wanategemea sana huruma ya Afrika Kusini kwa kushinda mchezo wao dhidi ya Nigeria huku wao wakitakiwa kushinda mchezo wao dhidi ya Sudan.

Ghana wanaojulikana kama Black Stars pamoja na kufungwa bao 1-0 na Uganda Jumamosi iliyopita lakini bado wanaendelea kuongoza kundi E wakiwa na alama nane na watahitaji sare yeyote katika mchezo wao dhidi ya Togo leo ili waweze kufuzu.

Kundi hilo bado liko wazi kwani Guinea na Uganda ambao wote wana lama saba bado nao wana nafasi ya kufuzu kama wakifanya vyema katika michezo yao mwisho.

Katika kundi D vita vikali vimebakia kati ya Ivory Coast na DR Congo ambao watagombea nafasi ya kufuzu moja kwa moja.

Ivory Coast ambao wana alama tisa tofauti ya alama tatu na DRC, watahitaji walau sare nyumbani dhidi ya Cameroon kesho ili waweze kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele.
Katika kundi B Mali, Malawi na Ethiopia watakuwa wakigombea nafasi moja iliyobakia ya kufuzu baada ya Algeria kuwa tayari wameshachukua nafasin ya kwanza.


Ratiba AFCON Novemba 19...muda kwa saa za Tanzania.


16:00SenegalvBotswana
17:00Ivory CoastvCameroon
17:00DR CongovSierra Leone
17:00GabonvLesotho
17:00EthiopiavMalawi
18:00MalivAlgeria
19:00GhanavTogo
19:00ZambiavCape Verde Islands
19:00NigervMozambique
19:00GuineavUganda
19:00ZambiavCape Verde
20:00NigeriavSouth Africa
20:00SudanvCongo
20:30TunisiavEgypt
21:00Burkina FasovAngola















0 comments:

Post a Comment