Thursday, 6 November 2014

Messi afikia rekodi ya Raul Ulaya.

Lionel Messi amefungana na nyota wa zamani wa Real Madrid Raul kwa ufungaji wa mabao mengi  katika Historia ya ligi ya mabingwa barani ulaya UEFA  baada ya Jana kufunga mabao yote 2 wakati Timu yake Barcelona inaichapa Ajax huko Amsterdam, Uholanzi.

Rekodi ya Raul ni mabao 71 na mabao hayo ya Messi yamemfanya afikishe mabao 71 huku nyuma yao akiwepo Mchezaji Bora Duniani Cristiano Ronaldo mwenye Mabao 70.

Mabao hayo ya Messi hapo Jana imeifanya Barcelona iungane na Bayern Munich, PSG na FC Porto kufuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCl huku zikiwa zimebakisha Mechi mbili za Makundi.

Wanaoshikilia rekodi ya mabao UEFA.

Lionel Messi  mabao 71
   
Raul  mabao 71

Cristiano Ronaldo  mabao 70
   
Ruud van Nistelrooy  mabao 56
   
Thierry Henry mabao 50

0 comments:

Post a Comment