Tuesday, 18 November 2014

Nchi 7 kujulikana Kesho kwenda AFCON 2015.

Afrika Kusini, Burkina Faso, Gabon, Cameroon, Cape Verde, Tunisia,Senegal na Algeria ni nchi zilifuzu michuano ya AFCON 2015  itakayochezwa mwakani huko Guinea ya Ikweta.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa wiki hii Katika kundi A Afrika Kusini walifuzu bada ya kuichabanga Sudan kwa mabao 2-1 huku Nigeria ambao nao wako katika kundi hilo wakifufua matumaini yao kwa kuifunga Congo Brazzaville kwa mabao 2-0.

Afrika kusini walifikisha alama 11 katika mechi tano walizocheza wakifuatia na Nigeria na Congo ambao wote wana alama saba huku Sudan wakiwa na alama tatu na kama Nigeria wakiifunga Bafana Bafana kesho  nao watakuwa wamejihakikishia nafasi hiyo.

Kundi B Algeria pamoja na kufuzu waliendelea ubabe kwa kuichapa Ethiopia kwa mabao 3-1 wakati Malawi wao waligaragaza Mali kwa mabao 2-0 na kuweka hai matumaini yao ya kufuzu. Kundi C Burkina Faso na Gabon zilijihakikishia nafasi yao ya kushiriki michuano hiyo ambapo Burkina Faso wao waliichapa Lesotho kwa bao 1-0 huku Gabon wao wakitoa sare ya bila ya kufungana na Angola.

Wengine waliofuzu na makundi wanayotoka ni Cape Verde kutoka kundi F ambao waliifunga Niger kwa mabao 3-0 wkati kundi G Tunisia nao walizosonga mbele pamoja na sare ya bila kufungana na Botswana huku Senegal nao wakiwaadhibu Misri nyumbani kwao wa bao 1-0.

0 comments:

Post a Comment