Mganda Lure kocha mkuu Stand United ya Shinyanga.
Klabu ya Stand United ya Shinyanga imefanya
marekebisho katika Benchi la ufundi baada ya kumchukua mwalimu Mathias Lure kutoka nchini Uganda kuwa kocha mkuu.
Lure ambaye mara ya mwisho alikuwa anaifundisha
klabu ya Express ya Uganda kama kocha mkuu,na alishawahi kuwa kocha wa timu ya
taifa ya vijana ya nchini humo.
Taarifa ya mtandao wa klabu hiyo imeeleza kuwa klabu
imeingia mkataba wa miezi sita na kocha huyo na ameshaanza kazi rasmi huku akisaidiwa na Emmanuel Massawe kocha msaidizi
wa kwanza na Athumani Bilali kocha msaidizi wa pili.
Ikumbukwe kuwa Dirisha dogo la usajili Tanzania limefungwa na STAND United imesajili
wachezaji wafuatao.
Haruna Chanongo kutoka Simba SC(Mkopo),Chinedu
Nwankoene (NIGERIA),Hamisi Thabiti Kutoka Yanga (Mkopo),Shaaban Kondo (Tessema
fc) inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara,Zuber Ubwa,mtanzania aliyekuwa
anacheza soka nchini Ureno katika timu ya daraja la pili.
Wengine ni Hamisi Shengo (mchezaji huru),msimu
uliopita alikuwa mchezaji wa Coastal Union ya Tanga Pamoja na Charles Mishetto aliyekuwa anacheza katika
ligi daraja la nne nchini ujerumani.
0 comments:
Post a Comment