Monday, 29 December 2014

VPL Mtibwa bado inashikilia nafasi ya kwanza,Ndanda inaburuza mkia.

Wakati raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imekamilika jana (Desemba 28 mwaka huu) kwa mechi tatu, ligi hiyo itaingia raundi ya tisa Januari 3 mwakani kwa mechi tano.

Coastal Union itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani, Ruvu Shooting itaikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Azam itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Azam Complex, Stand United itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri wakati Mbeya City na Yanga zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Sokoine.

Ligi hiyo ambayo itachezwa mfululizo (non-stop) hadi itakapomalizika Mei 9 mwakani, itakamilisha raundi ya tisa Januari 4 mwakani kwa mechi kati ya Mgambo Shooting na Simba kwenye Uwanja wa Mkwakwani, na Tanzania Prisons itakayokuwa mwenyeji wa Ndanda kwenye Uwanja wa Sokoine.
Katika michezo ya jana Yanga walitoshana nguvu na Azam kwa sare ya 2-2 huku Mbeya City ikishinda 1-0 dhidi ya Ndanda.

Mtibwa bado inashikilia nafasi ya kwanza ikiwa na alama 16 ikifuatiwa na Azam alama 14 Yanga nafasi ya tatu alama 14 tofauti ya magoli na Azam wakati Kagera Sugar inashikilia nafasi ya nne alama 13.

0 comments:

Post a Comment