Barcelona na Athletico Madrid kupambana kesho Copa Del Rey
Atletico Madrid na Barcelona watapambana kesho (Jumatano Usiku) huko Nou Camp kucheza Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe la Mfalme nchini Hispania Copa del Rey.Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita Atletico Madrid waliwatoa mabingwa watetezi klabu ya Real Madrid kwa Jumla ya Bao 4-2 katika Mechi mbili.
Atletico waliishinda Real Mechi ya kwanza 2-0 Nyumbani kwao Vicente Calderon na kutoka Sare 2-2 huko Santiago Bernabeu.
Barcelona wao waliitwanga Elche Jumla ya Bao 9-0 kwa Mechi mbili baada ya kushinda 5-0 Nou Camp na 4-0 kwenye Marudiano Nyumbani kwa Elche.
0 comments:
Post a Comment