VPL Leo ni vita kati ya Kagera Sukari na Azam fc.
Ligi kuu ya soka Tanzania Bara itaendelea tena leo kwa mchezo moja ambapo klabu ya Kagera Sukari itapambana na Azam fc kusaka alama tatu muhimu.Mechi hiyo ya kiporo ya ligi kuu Tanzania bara itapigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kagera Sukari inahitaji ushindi baada ya mchezo wa mwisho kufungwa 1-0 na Mbeya City jumamosi iliyopita.
Kwa upande wa Azam fc wanaingia kwenye mchezo wa leo wakijiamini kutokana na ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Stand United mwishoni mwa wiki iliyopita uwanja wa CCM Kambarage Shinyinga.
Baada ya hapo Azam itarudi jijini Dar es salaam kwenda kupambana na Simba jumamosi hii.

0 comments:
Post a Comment