Kikosi cha maboresho Taifa Stars Chatajwa.
Kocha wa timu ya taifa ya soka
Tanzania, Mholanzi Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26
kitakachoivaa Rwanda katika mechi ya kirafiki itakayochezwa Mwanza,hapo January
22.
Rwanda itakuwa mwenyeji wa fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani.
Walioteuliwa ni wachezaji waliochini ya miaka 22 wakiwa ni sehemu ya matayarisho ya kucheza timu ya taifa miaka ijayo.
Wachezaji hao na timu zao katika mabano ni
makipa Aishi Manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Peter Manyika (Simba)
Wakati mabeki ni Miraji Adam, Andrew Vincent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) Joram Mgeveke ( Mwadui), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Edward Charles (Young Africans).
Viungo ni Salum Telela ( Yanga) , Adam Salamba (Bulyankulu FC) wakati Hassan Banda, Mohammed Hussein, Said Makapu na Said Ndemla wakiwa ni wachezaji wa Simba Sports Club.
Viungo wengine ni Hussein Malombe (Geita Gold SC), Shiza Ramadhani (Mtibwa Sugar), Omar Nyenje (Ndanda FC), Hassan Dilunga (Yanga) na Alfredy Masumbakenda ( Bulyankulu SC).
Washambuliaji ni Aboubakar Mohammed (White Bird), Kelvin Friday (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Atupele Mwaisemba na Rashid Mandawa (Kagera Sugar).

0 comments:
Post a Comment