Messi ana kipaji zaidi ya Ronaldo asema Capello.
Kocha wa timu ya taifa ya Urusi, Fabio Capello amesema mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ana kipaji kikubwa zaidi kuliko mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo lakini anaamini magumu anayopitia nyota huyo wa kimataifa wa Argentina akiwa Camp Nou yanaweza kumletea matatizo katika miaka ijayo.Ronaldo alinyakuwa tuzo ya Ballon d’Or Jumatatu iliyopita kwa mara tatu na Capello amekataa kuondoa uwezekano wa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kushinda tena tuzo hiyo zaidi ya Messi ambaye ameinyakuwa mara nne.
Akiulizwa kama anadhani Ronaldo anaweza kushinda tuzo nyingi zaidi ya Messi, Capello alijibu kuwa Messi anakipaji kikubwa zaidi ya Roanldo lakini amekuwa akipata matatizo katika klabu yake jambo ambalo linaweza kuwa chanzo cha kumrudisha nyuma.
Capello aliendelea kudai kuwa Ronaldo kwasasa yuko fiti kiakili na kimwili huku akiwa anasaidiwa kwa karibu na wachezaji wenzake ndio maana nadhani anaweza kuendelea kuimarika na kushinda tuzo zaidi.
0 comments:
Post a Comment