Thursday, 29 January 2015

Kombe la Taifa wanawake nusu fainali leo.

NUSU fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Taifa la Wanawake inatarajiwa kurindima leo Dar es Salaam na kushirikisha timu nne zitakazomenyana kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, mechi za nusu fainali zote mbili zitachezwa leo na baada ya hapo kutakuwa na siku mbili za mapumziko ambazo ni kesho na keshokutwa kabla ya fainali itakayochezwa Jumapili.

Nusu fainali ya kwanza itaanza saa nane ambapo Pwani itamenyana na Kigoma na kabla ya Temeke kucheza na Ilala katika nusu fainali ya pili inayotarajiwa kuanza saa 11 jioni.

Temeke ilipata nafasi ya kushiriki hatua hiyo baada ya kuifunga Mbeya mabao 3-0 huku Ilala ikiilaza Iringa kwa mabao 2-0.

Aidha, timu ya Kigoma ilifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Mwanza mabao 2-1 huku Pwania wakikata tiketi ya nusu fainali kwa kuifunga Tanga mabao 5-2.
Chanzo Habari leo.

0 comments:

Post a Comment