Tottenham na Chelsea kupambana fainali ya Capital One.
Klabu ya Tottenham hotspur itapambana na Chelsea katika mchezo wa fainali kombe la Capital One baada ya kufuzu kwa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya Shieffield.Katika mchezo wa kwanza Tottenham ilipata ushindi wa bao 1-0 na jana ilitoka sare ya 2-2.
Christian Eriksen alifunga mabao yote ya Tottenham huku Che Adams naye akifunga mabao yote ya Shiffield.
Juzi Chelsea ilitinga fainali baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Liverpool.
Mchezo wa fainali utapigwa Machi mosi katika uwanja wa Wembely.
0 comments:
Post a Comment