Thursday, 29 January 2015

Zilizoingia Robo fainali AFCON zapatikana,Mali na Guinea kupangwa baadaye.

Timu ya taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika baada ya kushinda mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Cameroon kwa 1-0.

Bao pekee lililoipa Ivory Coast alama  zote tatu lilifungwa na mshambuliaji Max Alain Gradel ambaye alifunga bao hilo kwenye dakika ya 36 ya mchezo na kuihakikishia timu yake uhakika wa kusonga mbele .

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Ivory Coast wanafuzu kama washindi wa kwanza wa Kundi D wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama  5 baada ya kutoka sare kwenye michezo miwili na kushinda mchezo mmoja.

Ivory Coast watacheza mchezo wa robo fainali dhidi ya washindi wa pili wa kundi C ambao ni Algeria huku Ghana wakingoja kumfahamu mshindi wa pili wa kundi D.

Timu nyingine zilizoingia robo fainali ni Congo Brazavile,Congo Kinshasa,Tunisia,Wenyeji Guinea ya Ikweta.

0 comments:

Post a Comment