Sare zatawala AFCON mechi za jana,leo patashika.....
Timu ya taifa ya Zambia imelazimisha sare ya kufungana goli 1-1 na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) katika mechi ya kundi B ya mataifa ya Afrika iliyopigwa usiku wa jana.Bao la mapema la Given Singuluma (dakika ya 2') liliwaamsha mashabiki wa Chipolopolo, lakini katika dakika ya 66' kipindi cha pili Yannick Bolasie alisawazisha bao hilo.
Mechi ya pili iliyoanza majira ya saa 4:00 usiku, miamba ya soka kaskazini mwa Afrika, Tunia ilitoka sare ya 1-1 na Cape Verde.
Tunisia walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 70' kupitia kwa Mohamed Ali Moncer, lakini dakika ya 78' Cape Verde walisawazisha kupitia kwa Heldon aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.
Michuano hiyo itendelea tena leo ambapo Ghana itapambana na Senegal saa moja jioni huku Afrika ya kusini ikioneshana ubabe na Algeria kuanzia saa nne usiku
0 comments:
Post a Comment