Simba kuanza mazoezi kesho kwa ajili ya Azam.
Klabu ya Simba itaanza mazoezi kesho asubuhi kujiandaa mchezo dhidi ya Azam fc itakayopambana nayo katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara itayofanyika uwanja wa Taifa, Dar es salaam.Meneja wa Simba, Nico Nyagawa amesema kuwa kocha Goran Kopunovic alitoa mapumziko kuanzia jana jioni na leo baada ya ushindi wa mabao 2-0 waliopata jumamosi iliyopita dhidi ya Ndanda fc kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara.
Nyagawa amesema kuwa wataanza mazoezi kesho asubuhi, lakini bado hajathibitisha uwanja watakaotumia.
Mechi hiyo ya wikiendi itakuwa ya pili katika ligi kwa kocha Kopunovic ambaye mpaka sasa hajafungwa mechi yoyote tangu aanze kazi ya kuifundisha Simba katika michuano ya kombe la Mapinduzi na alifanikiwa kutwaa kombe hilo januari 13 mwaka huu kwa kuifunga Mtibwa Sugar penalti 4-3 katika mechi ya fainali.
0 comments:
Post a Comment