Wajue wachezaji ambao hawana kasi duniani lakini wana madhara makubwa dimbani.
Ni wachezaji gani hapa duniani ambao wanacheza soka safi lakini si ya kasi zaidi?Siku zote tunawazungumzia wachezaji wenye kasi zaidi lakini tumewasahau wanaocheza soka ambayo haina kasi lakini wana madhara makubwa sana wakiwa dimbani..
Wachezaji wasio na kasi dimbani kwa mujibu wa FIFA
Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha ya wachezaji ambao hawana kasi zaidi uwanjani lakini wana madhara makubwa sana pindi wakishika mpira.FIFA limetoa orodha ya nyota 10 bora katika mwaka 2014
10. Francesco Totti – Roma.

Ni wachezaji wachache wanaoweza kudumu na klabu mmoja kwa sasa hapa duniani.lakini kwa muitaliano imekuwa tofauti,amedumu na Roma kwa muda wa miaka 23. Totti Hana kasi uwanjani lakini hawezi kukosekana katika first eleven ya Roma kutokana na uwezo wake wa kuwatengenezea wenzake nafasi ya kufunga mabao.
9. Emile Heskey – Bolton Wanderers

Emile Heskey mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool amecheza mechi 150 akiwa na Liverpool amecheza ndani ya Leicester, Birmingham, Wigan na Aston Villa akiwa katika ligi kuu ya Uingereza na amecheza mechi 62 akiwa na timu ya taifa ya England.kwa sasa ameniunga na
Bolton Wanderers baada ya kutangaza kurudi tena dimbani.
8. Andrea Pirlo – Juventus

Ingawa hana kasi dimbani, Andrea Pirlo anajulikana kama mmojawapo wa viungo bora dunian. Pirlo mwenye miaka 34 ni mchezaji wa tano kucheza mechi nyingi akiwa na timu ya taifa ya Italia .Amecheza mechi 400 amebeba UEFA kwa upande wa vilabu mara mbili akiwa na AC Milan.
7. Gareth Barry – Everton

Gareth Barry ni mmojawapo kati ya nyota wenye spidi ndogo ligi kuu Uingereza,Barry ana uwezo mkubwa wa kucheza mpira na amecheza mechi 500akiwa na Aston Villa na Manchester City.
0 comments:
Post a Comment