Yanga yaanza mawindo Kwa ajili ya Ruvu Shooting.
Klabu ya Yanga imeingia kambini jana kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu bara dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumamosi ya wiki hii.Klabu hiyo inatarajiwa kwenda Lusaka, Zambia kushiriki michuano maalumu itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Ofisa Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro alisema kuwa timu hiyo ilialikwa kushiriki michuano hiyo na tayari imeshapata ruhusa ya kushiriki kutoka kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF).
Yanga inawakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuanza mwezi ujao hivyo michuano hiyo ya Lusaka itakuwa msaada mkubwa kwenye maandalizi.
Murro alisema, awali kocha Mkuu wa timu hiyo Mholanzi Hans van der Pluijm alihitaji mechi za kirafiki za kimataifa ili kukipima kikosi chake, hivyo walivyopata mwaliko huo wa Zambia waliona ni nafasi nzuri kwao.
Alisema timu ipo kwenye maandalizi na kwamba inatarajiwa kwenda Zambia baada ya kucheza mechi mbili za kirafiki na kwamba michuano hiyo inatarajiwa kuanza Januari 28 mpaka Februari 4.

0 comments:
Post a Comment