Friday, 30 May 2014

Wenger asaini mkataba ndani ya Arsenal,kumaliza na Van Gaal

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ametia saini mkataba wa miaka mitatu katika  klabu hiyo hadi mwaka 2017.
Wenger mwenye miaka 64, ameongoza Arsenal na kufanikisha ushindi wa mataji 8 tangu kujiunga na klabu hiyo Septemba mwaka 1996,imeelezwa na Supersports.com
"Wenger amekuwa na Arsenal kwa  miaka 17, na hii imemfanya awe kocha aliyetumikia klabu kwa muda mrefu katika historia yetu," imeeleza taarifa katika mtandao wa Arsenal.
Msimu huu aliweza kuongoza timu hiyo hadi kufuzu kwa mara ya 17 kwa kombe la klabu bingwa ulaya na kupata ushindi aliosubiri kwa hamu kwa miaka tisa dhidi ya Hull City katika fainali ya kombe la FA Cup.
Arsenal ilikuwa haijawahi kushinda taji la nyumbani tangu mwaka 2005 ingawa walifika fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya mwaka 2006.

Wenger, ambaye sasa ni kocha  mkongwe zaidi katika ligi ya Ulaya baada ya Sir Alex Ferguson kustaafu, mwezi Mei mwaka 2013, anasifika kwa kuleta mawazo mapya kuhusu michezo na lishe bora katika soka Uingereza. 

Kwa maana hiyo Wenger atamaliza mkataba wake na kocha wa Manchester United Louis Van Gaal.

''Huyu ndiye mtu anayefanya kazi mwa saa 24 kila siku,'' alisema mlinda lango wa zamani wa Arsenal Bob Wilson.
"anachukia sana kushindwa. Alileta mageuzi makubwa, katika kila sekta ya mchezo huo nchini Uingereza. Watu wanadhani kuwa ana mamlaka sana lakini mtu ambaye anajitolea sana kwa mchezo huu ni mtu anayethaminiwa sana.''
Ushindi mkubwa wa Wenger ulikuwa wakati ambapo alishinda kombe la ligi ya Uingereza kati ya mwaka 2003-04 alipokuwa na wachezaji kama vile Thierry Henry na Patrick Vieira.
Wenger alimsajili Mesut Ozil kwa kima cha dola milioni 42.4 kwa msimu ambao umekamilika.
Lakini licha ya hali ya suitofahamu kuhusu mustakabali wa Wenger mwezi Januari, mkurugenzi mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alitabiri kuwa Wenger huenda akaongezewa muda Arsenal.
  • Rekodi ya Wenger

    Ligi ya Premier:1998, 2002, 2004
  • Kombe la FA:1998, 2002, 2003, 2005, 2014
  • Kombe la Community Shield:1998, 1999, 2002, 2004
  • Kombe ya ligi ya klabu bingwa nafasi ya 2: 2006
  • Nafasi ya pili kombe la Uefa Cup:2000
  • Nafasi ya pili Kombe la League:2007, 2011

0 comments:

Post a Comment