Taifa stars kucheza na Malawi
Taifa Stars na Malawi (Flames) zinapambana Jumanne (Mei 27 mwaka huu) katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.
Mechi hiyo itakuwa ya mwisho kwa Taifa
Stars kujipima kabla ya kucheza mchezo wa marudiano wa michuano ya
Afrika na Zimbabwe (Mighty Warriors) utakaofanyika Juni Mosi mwaka huu
jijini Harare.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager ipo kambini Tukuyu mkoani Mbeya chini ya Kocha wake Mart
Nooij kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi na ile ya Zimbabwe.
Malawi imewasili jana mchana (Mei 24
mwaka huu) kwa ndege ya Malawian Airlines kwa ajili ya mchezo huo ikiwa
na msafara wa watu 27, na imefikia kwenye hoteli ya Sapphire Court
iliyopo Mtaa wa Lindi jijini Dar es Salaam.
Flames inayofundishwa na mchezaji wa
zamani wa kimataifa wa Malawi, Young Chidmozi imefanya mazoezi jana jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Baada ya mechi hiyo, Malawi itakwenda
moja kwa moja nchini Chad kwa ajili ya mechi ya marudiano ya michuano ya
Afrika itakayochezwa Mei 30 mwaka huu jijini Ndjamena.
0 comments:
Post a Comment