Huyu ndiye bingwa mpya wa mieleka mwaka 2014,awagaragaza wanaume 7,Randy aumizwa

John Cena aliwashinda wanamieleka Kane,Roman Reigns, Randy Orton, Bray Wyatt, Bingwa wa Marekani Sheamus, Cesaro na Alberto Del Rio katika mchezo huo unaohusisha ngazi ili kumpata bingwa mpya wa uzito wa juu duniani.
Hapo kabla bingwa anayemiliki mkanda huo Daniel Bryan alijitoa rasmia June 9 baada ya kutopona vema na bado hajakamilisha matibabu yake.
Katika mchezo wa jana Orton alipigwa ngazi kichwani na kuchanika na kumfanya aumie vibaya lakini madakatari walimpa matibabu ambapo ameshonwa nyuzi kadhaa.
Money in the bank ni mchezo ambao wanamieleka hupigana na kisanduku kufungwa juu na kuning'inia na atakayeshinda ataweka ngazi ili atoe mkanda huo na ndipo atakuwa mshindi,na hivyo ndivyo alivyofanikiwa John Cena .
Matokeo mngine jana
Rusev alishinda kwa Big EKikundi cha Stardust & Goldust kilishinda mbele ya RybAxelSeth Rollins amabaye alijitoa kutoka kikundi cha shield aliwapiga Dean Ambrose, Dolph Ziggler, Jack Swagger, Kofi Kingston na Rob Van Dam) na kushinda mkanda mwingine wa money in the bank kwa upande wa mkataba.
Adam Rose alishinda mbele ya Damien SandowMabingwa kwenye kipengele ya timu ya muungano,mapacha Usos walishinda mbele ya The Wyatt Family
Kwa mambo mengine yanmayojiri usikose kufuatilia mtandao huu Sports4lifetz
0 comments:
Post a Comment