Morata atua Juventus.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata, amekamilisha Uhamisho wa kwenda Juventus kwa Dau la Euro Milioni 20.
Lakini Mkataba wa Uhamisho wa Mchezaji huyo mwenye Miaka 21 una kipengele kinachoiruhusu Real kumnunua tena kwa Dau linaloweza kufikia Euro Milioni 30 ikitegemea na Mechi atakazochezea Juventus.
Akizungumzia Uhamisho wake, Morata amesema: “Nimekuja kwenye Klabu hii kwa sababu ina Historia kubwa Ulaya na Duniani na, bila shaka, ndio bora Italia.”
Pia alisema kuwa kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, ambaye ni Raia wa Italia, amemtakia heri na kumwambia ajisikie raha Italia na pia kufurahia chakula chake.
Alipoulizwa kama mabadiliko ya kocha ndani ya Juventus yaliyofanywa Juzi baada ya kuondoka Antonio Conte na kuteuliwa Massimiliano Allegri kama yamemuathiri, Morata alijibu: “Nimeongea na Allegri Leo na nina shauku kuanza kazi. Klabu imeonyesha imani kubwa kwangu na nina imani na Watu wa hapa.”
Morata anakuwa Mchezaji wa pili kutoka Hispania kujiunga na Juventus katika Miezi 13 iliyopita kufuatia kujiunga kwa Fernando Llorente.
Na Morata ametamka: “Kucheza na kina Tevez, Vidal, Pirlo na Llorente ni kitu chema kabisa. Kuwa miongoni mwa Mastraika watatu bora ni kitu safi kwa Timu kwani ushindani utanifanya nifanye bidii zaidi!”

0 comments:
Post a Comment