Thursday, 3 July 2014

Majina ya Waamuzi wa robo fainali kombe la dunia

Shirikisho la soka duniani FIFA limetangaza Majina ya waamuzi watakaochezesha Mechi za Robo Fainali za Kombe la Dunia,Brazil 2014.
Waamuzi  waliotangazwa ni michezo ya Ufaransa v Ujerumani, Brazil v Colombia
Michezo hiyo itapigwa kesho julai 4, 2014
Nestor Pitana
Mechi ya kwanza ya Ijumaa kati ya Ufaransa na Ujerumani,Nestor Pitana atasimamia  na hii itakuwa ni Mechi ya 4 kwa mwamuzi   huyo kutoka Argentina kuchezesha huko Brazil.
Pitana, mwenye Miaka 39, alichezesha Mechi za Makundi huko Brazil kati ya Urusi na Korea , Marekani na Ureno na Honduras dhidi ya Switzerland.
Mechi ya Wenyeji Brazil na Colombia itachezeshwa na mwamuzi wa Hispania Carlos Velasco.
Carlos Velasco
Velasco, mwenye Miaka 43, amebahatika kusimamia Mechi 2 huko Brazil ambazo ni zile za Makundi kati ya Uruguay na Uingereza na ile ya Bosnia and Herzegovina dhidi ya Iran.

0 comments:

Post a Comment