Thursday, 3 July 2014

Robo fainali kombe la dunia kuanza kesho

Robo fainali za Kombe la Dunia zitachezwa kesho (Julai 4) na keshokutwa (Julai 5) huko Brazil na Timu 8 zinasaka nafasi 4 za kuingia Nusu Fainali.
Timu zilizoingia rovo fainali ni  Wenyaji Brazil, ambao ni Mabingwa wa Dunia mara 5, wapo Mabingwa wengine wa zamani Ufaransa,Ujerumani na Argentina lakini pia zipo timu ambazo hazijawahi kutwaa Kombe hili ambazo ni Colombia, Ubelgiji,Uholanzi na Costa Rica.

Brazil iliingia robo fainali baada ya kuitoa Chile kwa mikwaju ya pelnati vilevile Ujerumani iliitoa Algeria katika muda wa nyongeza wakati Ubelgiji nao iliwachukua mpaka muda wa nyongeza kuwatoa Marekani.
Aidha Costa Rica mikwaju ya pelnati  iliwapeleka hatua hii baada ya kuwafunga Ugiriki.
Uholanzi na Ufaransa waliingia baada ya kushinda katika dakika 90 za mchezo,Uholanzi ikiwatoa Mexico wakati Ufaransa iliwachomoa mabingwa wa Afrika Nigeria.

Ratiba kamili ya robo fainali mpaka fainali.
IJUMAA, JULAI 4, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Ufaransa v Ujerumani [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

2300
Brazil v Colombia [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza

JUMAMOSI, JULAI 5, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Argentina v Ubelgiji [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia

2300
Uholanzi  v Costa Rica [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador

NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi kati ya Ufaransa  v Ujerumani v Mshindi Brazil v Colombia [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte

JUMATANO, JULAI 9, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi kati ya Argentina v Ubelgiji v Mshindi kati ya Uholanzi v Costa Rica [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo

MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Aliyefungwa 61 v Aliyefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia

FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

0 comments:

Post a Comment