Wednesday, 16 July 2014

Manchester United imekula kwao,Martins Indi miaka minne ndani ya Porto.

Mlinzi wa timu ya taifa ya Uholanzi Bruno Martins Indi amejiunga na klabu ya FC Porto akitokea Feyenoord  kwa mkataba wa miaka minne,klabu hiyo imetangaza rasmi.
Mchezaji huyo mwenye miaka  22 amesema kuwa anafuraha sana kujiunga na klabu hiyo,kupitia mtandao wa klabu (www.feyenoord.nl).
"Nimecheza michezo zaidi ya  100 nikiwa na  Feyenoord na sasa jina langu limekuwa kubwa dunia nzima kupitia kombe la dunia ,timu yangu itafaidika pia ila naenda kupambana na changamoto mpya kule Ureno." alisema Indi.
Beki huyo mahiri alikuwa anawindwa na Manchester United kwa muda mrefu lakini ni wazi Van Gaal kocha mpya wa Manchester United atakosa huduma ya Indi.
Martins Indi alizaliwa Ureno,wazazi wake wanatokea  Guinea Bissau lakini akiwa mdogo alikulia Uholanzi.Amecheza michezo  22 akiwa na timu ya taifa ya Uholanzi.

0 comments:

Post a Comment