Monday, 25 August 2014

Algeria imesimamisha soka wikiendi hii baada ya mchezaji kuuawa

Taarifa kutoka nchini Algeria zinadai kuwa Algeria  imesimamisha shughuli sa soka wikiendi hii ili iwe kumbukumbu kwa mchezaji Albert Ebosse, aliyeuawa siku ya jumamosi.
Mchezaji huyo raia wa Cameroon mwnye miaka 24 amefariki dunia akiwa hospitali baada ya kupigwa na kitu kilichorushwa kutoka jukwaani wakati wa mechi ya Ligi ya Algeria, timu yake JS Kabylie ikicheza na USM Alger mjini Tizi Ouzou.
Taarifa zilizonaswa na Sports4lifetz zinaeleza kuwa  Shirikisho la soka nchini Algeria(AFF) limetangaza kusimamisha shughuli za soka kwa muda usiojulikana.
Naye rais wa shirikisho la soka la Algeria Mahfoud Kerbadj aliyekwepo uwanjani amesema mauaji hayo ni jambo la hatari nchini Algeria. AFF limetoa kiasi cha  $100,000 ili iwe rambirambi.
Wakati huohuo Rais wa  Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Issa Hayatou Amesema kuwa uchunguzi ufanyike mara  moja.
Hayatou amesema kuwa hatua kali zichukulie dhidi ya uhalifu huo uliofanyika na kuongeza kuwa uhalifu huo haukubaliki barani Afrika.
Msimu wa mwaka 2013-14 Ebosse alimaliza akiwa mfungaji bora akiwa amefunga mabao  17 na juzi aliifungia bao Kabylie katika mechi hiyo iliyoisha kwa kipigo cha nyumbani cha 2-1 kutoka kwa USM Alger.

0 comments:

Post a Comment