Diego Simeone afungiwa mechi 8 huko Hispania.
Shirikisho la soka nchini Hispania(SFF) limemfungia mechi 8 kocha mkuu wa klabu ya Atletico Madrid,Diego Simeone baada ya kutolewa nje katika mchezo wa marudiano Super Cup dhidi ya Real Madrid.Taarifa iliyotangazwa muda mfupi uliopita na shirikisho hilo imekuja baada ya siku tatu kupita baada Atletico kuwafunga Real Madrid bao 1-0 na hivyo kubeba kombe la Super Cup kwa jumla ya mabao 2-1.
Simeone amefungiwa mechi nne kwa kosa la kuvuka mstari akiwa karibu na mwamuzi msaidizi na mara mbili alionekana akimgonga Refa huyo nyuma ya Kichwa, michezo miwili baada ya kugoma kutoka, mchezo moja baada ya kupiga makofi wakati akipewa adhabu hiyo na mchezo moja kwa kosa la kubaki uwanjani kwa muda badala ya kutoka uwanjani baada ya vurumai hiyo.
Kocha msaidizi German Burgos atachukua mikoba ya Simeone wakati anatumikia adhabu hiyo.


0 comments:
Post a Comment