Wednesday, 13 August 2014

Kombe la Kagame Azam yabanwa mbavu.

Mashindano ya vilabu bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama kombe la Kagame yanaendelea mjini Kigali.
Timu ya Azam Fc ya Tanzania imetoka sare ya kufungana magoli 2-2 na Atlabara ya Sudan Kusini katika katika mashindano ya kombe la Kagame .
Mechi ilichezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali siku ya jumanne.
Azam wameongoza mchezo na kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa goli 1 lililotiwa kimiani na mshambuliaji Balou kunako dakika ya 44.
Goli hilo lilikombolewa na mshambuliaji Thomas kunako dakika ya 48 kabla ya Martin Bonny kufunga goli la pili la Atlabara kunako dakika ya 54
Azam imesubiri dakika ya 85 kumuona mshambuliaji wake Kavumbagu akirudishia matumaini ya angalau kupata alama moja.
AZAM inaongoza kundi la A ikiwa na alama 5 ikifuatiwa na Rayon Sport ya Rwanda yenye alama 4.
Mechi iliyotangulia imeshuhudia sare ya goli moja kati ya timu ya Adama City ya Ethiopia na KMKM ya Zanzibar.
Leo (jumatano)pia zitachezwa mechi mbili KCC ya Uganda itamenyana na Atletico ya Burundi huku APR ya Rwanda ikizipiga na Telecom ya Djibuti.
Police FC ya Rwanda ndiyo timu pekee iliyokwisha jihakikishia tiketi ya kufuzu katika robo fainali hata kabla ya mechi za mchujo kumalizika.
Chanzo BBC

0 comments:

Post a Comment