Lampard atamatisha soka la kimataifa.
Kiungo muingereza Frank Lampard ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya kuichezea timu ya taifa ya Uingereza michezo 106.Kiungo huyo huyo wa zamani wa Chelsea, mweye miaka 36, aliyejiunga na Manchester City kwa mkopo akitokea New York City, alicheza mechi yake ya mwisho kama nahodha wa Uingereza katika suluhu ya 0-0 dhidi ya Costa Rica katika michuano ya Kombe la Dunia, mwezi Juni.
Lampard alianza kucheza soka na timu ya Uingereza Oktoba mwaka 1999, alipocheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Ubelgiji.
Lampard amecheza katika michuano mitano mikubwa na kupachika mabao 29.
Anakuwa mchezaji wa sita kuwahi kuichezea England mara nyingi zaidi sawa na Sir Bobby Charlton. Lampard, aliyeanza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya West Ham, aliondoka Chelsea msimu uliopita baada ya kuichezea klabu hiyo mara 648 na kufunga magoli 211.
Akitangaza hilo Lampard amesema kuwa anafurahi kucheza soka kwa muda huo wote na sasa ataweka majukumu yake zaidi ndani ya klabu yake.
Mwishoni mwa Msimu uliopita, Chelsea iligoma kumuongezea Lampard Mkataba na yeye akaamua kwenda Marekani kwenye MLS na kujiunga na Klabu mpya New York City FC ambayo ni Klabu inayomilikiwa na Man City.
Mwezi uliopita nahodha wa Uingereza Steven Gerrard alitangaza kustaafu soka la kimataifa.
0 comments:
Post a Comment