Rasmi Di Maria asaini na kukabidhiwa jezi namba 7 ndani ya Man U.
Klabu ya Manchester United imetangaza rasmi kuwa Ángel Fabián Di María Hernández amekamilisha Uhamisho wake kwa Dau la Rekodi huko Uingereza la Pauni Milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Hispania.Mara baada ya kukamilisha taratibu za Uhamisho, Di Maria alisema kuwa ana furaha sana ya kujiunga na Manchester United.
Di Maria ameongeza kuwa alikuwa naraha kule Hispania na Klabu nyingi zilimhitaji lakini Man United ndio Klabu pekee angeweza kuiacha Real Madrid ili kujiunga nayo.
Kuhusu Louis van Gaal,Di Maria alisem"ni Kocha bora sana mwenye rekodi nzuri na nimevutiwa mno na dira na nia ya kila Mtu Klabuni hapa ili kuirudisha tena juu ambako ndiko inastahili kuwepo pia nina hamu kubwa kuanza kazi!”
Kwa upande wake kocha Louis van Gaal, akimkaribisha Di Maria, amesema: “Angel ni Kiungo wa kiwango cha Dunia lakini muhimu zaidi ni Mchezaji Kitimu. Hamna shaka kuhusu kipaji chake kisicho mfano. Ni mwepesi sana na hatari kwa Guu la Kushoto ambae anatisha Difensi yoyote ile. Uwezo wake kukokota Mpira na kuwakabili Mabeki na kuwadaa ni kitu cha furaha kukiangalia. Ni nyongeza safi sana kwa Timu!”
Ujio wa James Rodriguez na Toni Kroos ndani ya Madrid umehamasisha zaidi Di Maria kujiunga na Manchester United.
Di Maria atavaa jezi namba 7 ndani ya Man U jezi ambazo zimevaliwa na nyota David Beckham, Eric Cantona, Cristiano Ronaldo, George Best na Bryan Robson.
Wasifu wake
| Jina kamili | Ángel Fabián Di María Hernández | ||
|---|---|---|---|
| Kuzaliwa | 14 February 1988 | ||
| Sehemu alipozaliwa | Rosario, Argentina | ||
| Nafasi uwanjani | Winga / kiungo mshambuliaji | ||
| Vilabu | |||
|
Kwa sasa
|
Manchester United | ||
| Namba | 22 | ||
| Vijana | |||
| 1995–2005 | Rosario Central | ||
| wakubwa | |||
| Mwaka | Team | Amecheza mara | (mabao) |
| 2005–2007 | Rosario Central | 35 | (6) |
| 2007–2010 | Benfica | 76 | (7) |
| 2010– | Real Madrid | 124 | (22) |
| Timu ya taifa | |||
| 2007 | Argentina U20 | 13 | (3) |
| 2008 | Argentina U23 | 6 | (2) |
| 2008– | Argentina | 52 | (10) |

0 comments:
Post a Comment