Sunday, 14 September 2014

Coast Union kucheza na Mtibwa mkwakwani leo.

Timu ya Coastal Union ya Tanga  leo  Jumapili itacheza mechi ya kirafiki na Mtibwa Sugar  kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania
bara ambao unatarajiwa kuanza Septemba 20 hapa nchini.


Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na tayari walishafanya mazungumzo na uongozi wa wakata miwa hao hivyo Wameshawasili.
 Huo ni mchezo wa pili kwa Coastal Union kucheza Tanga  baada ya kurejea kutoka Visiwani Pemba ilipokuwa imeweka kambi ya mwezi mmoja kwa ajili ya matayarisho ya ligi kuu soka Tanzania bara.

Amesema baada ya mchezo wa kwanza timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Morogoro hivyo waliona umuhimu wa mechi hiyo lengo likiwa kukipa makali kikosi hicho kabla ya kuwavaa wekundu wa
msimbazi Simba siku ya ufunguzi wa Ligi kuu.

Ameongeza kuwa wanategemea mechi hiyo itakuwa na upinzani mkubwa sana hivyo wakazi wa Tanga na vitongoji vyake watumia fursa hii kuja kuiona timu yao ya Coastal Union ikipambana kwenye mchezo huo kabla haijaanza msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.
Hata hivyo amesema kuwa msimu huu timu hiyo imepania kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi zake za nyumbani na ugenini ili kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara .

0 comments:

Post a Comment