Cameroon kuandaa AFCON 2019,Ivorycoast ni 2021
Nchi za Cameroon, Ivory Coast na Guinea zimetajwa kuwa wenyeji wa michuano mikubwa barani Afrika yaani AFCON na shirikisho la soka barani Afrika katika mkutano uliofanyika jana jumamosina Ivory Coast AFCON za mwaka 2021.
Hata hivyo CAF ilitangaza kuwa Guinea ndiyo itakayokuwa mwenyeji wa makala ya 2023 kinyume na matarajio ya wengi.
CAF iliamua kuwatunuku Guinea uwenyeji wa mashindano hayo kabla ya kukamilika kwa muda uliowekwa kwani Guinea ilikuwa imeonesha nia ya kuandaa makala hayo jambo ambalo liliisaidia kuzipiku Algeria na Zambia ambazo zilikuwa zinawania uwenyeji huo.
Cameroon, itakuwa inaandaa makala hayo kwa mara ya pili baada ya kuwa mwenyeji wa makala ya 1972 ya mashindano hayo ya Afrika.
Kulingana na taarifa ya CAF ,Cameroon,inalenga kutumia viwanja vya Bafoussam, Douala, Garoua na Yaounde kufanikisha awamu hiyo ya mashindano.
Furaha hiyo ya kutuzwa kuwa wenyeji wa mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika ilitanda hadi Ivory Coast, ambayo imeratibiwa kuandaa makala ya mwaka wa 2021.
Hii vilevile itakuwa mara ya pili kwa taifa hilo kuwa mwenyeji wa mchuano huo baada ya kuandaa kipute cha mwaka wa 1984.
Ivory Coast imeratibu kuandaa mashindano hayo katika miji ya Abidjan, Bouake, Korhogo, San Pedro na mji mkuu wa Yamoussoukro.
Guinea haijawahi kuandaa mashindano haya katika historia yake ya miaka 57.
Makala ya kwanza ya kombe la mataifa bingwa Afrika yaliandaliwa katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.
Katika ombi lao kamati andalizi ya Guinea inapanga kuandaa mashindano hayo katika miji ya Conakry, Kankan, Labe na Nzerekore .
Kenya, Algeria, Ethiopia, Ghana, Mali na Zimbabwe zinawania kuandaa makala ya 2017 baada ya Libya kujiondoa kufuatia kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Septemba 30.
0 comments:
Post a Comment