Waandaaji wa AFCON 2019 na 2021 kujulikana leo au kesho.
Nchi tano na matoleo mawili ya michuano ya Mataifa ya Afrika ndio masuala yatakayolengwa zaidi na Shirikisho la Soka barani Afrika wakati kutakapopigwa kura za kuamua nchi wenyeji wa michuano ya mwaka 2019 na 2021.Kamati ya utendaji ya CAF itafanyia tathmini ya mwisho uwasilishaji kutoka nchi za Algeria, Cameroon, Ivory Coast, Guinea na Zambia katika kugombea nafasi ya kuandaa fainali za mwaka 2019 wakati Algeria, Ivory Coast na Guinea zikipambana tena kutaka nafasi ya kuandaa fainali hizo mwaka 2021.
Uamuzi unatarajiwa kutolewa nchini Ethiopia huku wajumbe 14 wakiwa na haki ya kupiga kura moja na mshindi atatakiwa kupata kura zisizopungua nane. Mshindi atatangazwa katika hafla itakayofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Afrika-AU jijini Addis Ababa. Zambia waliwahi kupewa nafasi ya kuandaa michuano hiyo mwaka 1988 lakini walishindwa na nafasi yao kuchukuliwa na Morocco kutokana na kushindwa kumudu gharama za maandalizi.
Safari hii Zambia inaonekana imejipanga vyema kwani imepeleka viwanja sita ukiwemo wa Livingstone mji ambao unatizamana na maporomoko ya mto Zambezi ambao ndio unaozigawa Zambia na Zimbabwe.

0 comments:
Post a Comment