Sunday, 14 September 2014

Mbeya City yatandikwa 4-1 na Vipers.

Klabu ya Mbeya City fc wametandikwa mabao 4-1 na Vipers FC (Zamani Bunamwaya) inayoshiriki ligi ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki uliopigwa jana  uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Vipers FC waliwasili jana asubuhi jijini humo.

Mechi hiyo ni ya mwisho ya kujipima ubavu kwa kocha Juma Mwambusi ambaye  ana changamoto ya kufanya vizuri katika msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Mwambusi aliyeibuka kuwa kocha bora msimu uliopita, anasaidiwa na Suleiman Jabiri baada ya msaidizi wake Maka Mwalwisyi kukataa kuongeza mkataba muda mfupi baada ya ligi kuu msimu uliopita kumalizika.

Maka kwasasa ni kocha mkuu wa klabu ya Panone FC ya mkoani Kilimanjaro na inashiriki ligi daraja la kwanza.
Mbeya City msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na mabingwa Azam fc.
Mbeya city wataanza kampeni ya ligi kuu msimu wa 2014/2015 kwa kuwakaribisha JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, septemba 20 mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment