VPL 2017/18 kuanza leo
Ligi kuu soka TANZANIA BARA kwa msimu wa 2017/18 Itaanza kutimua vumbi leo katika viwanja saba tofauti hapa nchini.
Mabingwa wa ngao ya jamii na michuano ya kombe la shirikisho SIMBA wataanza kutupa karata yao ya kwanza kupambana na RUVU SHOOTING,uwanja wa taifa DAR ES SALAAM.
Mbao watakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Majimaji ya Songea itakayosafiri hadi Mbeya kucheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo huku Njombe Mji ikiialika Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba huko Makambako.
Kadhalika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani, Mtibwa mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar itaikaribisha Stand United ya Shinyanga kwenye mchezo mwingine wa VPL ilihali Azam atakuwa mgeni wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mwadui watakuwa wenyeji wa Singida United ya Singida kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga na Jumapili kutakuwa na Mchezo mmoja utakaokutanisha Young Africans na Lipuli kwenye Uwanja wa Uhuru jijini
Wakati huohuo shirikisho la soka nchini Tanzania- TFF imesema Ni msimu mpya utakaotoa timu bingwa mpya itakayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), msimu wa 2019.
Itakumbukwa, msimu wa CAF wa 2018, timu itakayoiwakilisha nchi ni Young Africans SC ambayo ni Bingwa wa VPL msimu 2016/17 wakati michuano ya Kombe la Shirikisho, Tanzania itawakilishwa na Simba SC.
TFF inazitakia kila la kheri timu zote zinazoshiriki ligi hii, ikiamini kwamba uadilifu utaongoza mbele ya taratibu, kanuni na sheria zinazosimamia mpira wa miguu hapa nchini na kwingineko.
Read More